WANANCHI MKOANI KIGOMA WATAKIWA KUEPUKA MSONGO WA MAWAZO

Posted on: September 11th, 2025

Wananchi mkoani Kigoma washauliwa kuepuka msongo wa mawazo au sonona ili kuzuia uwezekano wa kupata ugonjwa wa akili, huku Dokta Ellen Mbekenga kutoka Hospitali ya Rufaa Maweni - Kigoma kitengo cha Afya ya akili akisisitiza kuhusu athari za msongo wa mawazo katika afya ya akili.

Mbekenge amesema hayo kupitia kipindi cha Good morning Joy FM na kuelezea baadhi ya sababu zinapelekea kupata msongo wa mawazo moja wapo, ikiwa ni uchumi pale mtu anapata changamoto za kuyumba kwa uchumi, Pili ikiwa ni Elimu hasa suala la masomo pale mtu anapokuwa amefeli katika masomo na kupelekea sonona, tatu ikiwa ni Familia (migogoro kwenye ndoa) pia matukio ya kimaisha kama kifo.

“Hakuna afya bila Afya ya akili sasa kuna sababu zinapelekea mtu kuwa na msongo wa mawazo au sonona sasa sababu hizi ni kama, uchumi, pale mtu anapotata changamoto ya kuporomoka kwa uchumi kumpelekea kuwaza namna gani anaweza kuishi, pili ni Elimu, katika masuala ya elemu hasa kwa wanafunzi pale anapokuwa amefanya vibaya mtihani yaken kumpelekea kupata sonona, tatu ni familia hasa masuala ya ndoa, pia matukio ya kimaisha kama kifo.” Amesema Mbekenge.

Aidha, Dkt Mbekenge amefafanua kuhusu kundi kubwa ambalo linathiriwa na ugonjwa wa Afya ya akili hasa mkoani kigoma ikiwa ni wanawake, na moja ya sababu zinapelekea wanawake kupata msongo wa mawazo au sonona ni matatizo katika familia, kwani Mwanamke ni nguzo ya familia pili ikiwa ni uzazi na tatu ikiwa Hedhi.

“ Moja ya kundi ambalo linakumbwa na sonona au Afya ya akili ni wanawake kwa sababu wanawake ni watu ambao wanahakikisha familia inapata mahitaji yote muhimu, changamoto zinazopelekea ni kama uzazi , Hedhi na familia” Amesema Mbekenge.

Sambamba na hayo, amelezea madhara ya ugonjwa wa afya ya akili ikiwa ni kushindwa kutimiza ndoto au malengo ambayo mama, baba, kijana au mtu yoyote anajiwekea, kushuka kwa kipato au uchumi katika familia, kujizulu au kujinyonya na kutoshirikiana na jamii katika kuzalisha na kushikamana .
“ kuna madhara mengi sana ya sonona ambayo yatampata mtu ikiwa atakosa msahada wa familia au jamii kumuweka sawa kiakili ili kuepusha sonona, moja ya madhara ikiwa ni kushindwa kutimiza ndoto zake pili kushuka kwa uchumi