WAKUU WA VITENGO WATAKIWA KUTIMIZA MAJUKUMU YAO
Posted on: September 12th, 2025
Leo tarehe 22 Agost, 2025 Idara ya utawala Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma imefanya kikao kwa lengo la kujadili masuala mbalilimbali likiwemo la utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2025/2026 pamoja na suala la ushirikiano katika mambo ya kijamii, maafa na changamoto zingingine baina yao.
Akizungumza katika kikao hicho mwenyekiti wa kikao Audax Lukiza ambaye pia ni Katibu wa Afya wa Hospitali amewataka watumishi wote katika idara ya utawala kujiunga katika kikundi cha M-Koba ili kuweza kuunganisha nguvu na umoja katika kusaidiana huku akisisitiza kuwa lengo la kikundi hicho ni kusaidiana na sivinginevyo.
"Wajumbe tuwambie tu kuwa huu umoja ni kwa ajili ya kusaidia katika maatatizo yanayo tukumbuka kama wana utawala hivyo tujiunge na kikundi hiki kwani kitaturahisishia sisi wenyewe namna ya kushikano mkono katika mambo mbalimbali ikiwemo maafa pamoja na sherehe”amesema Audax.
Aidha Mwt. Audax amendelea kusisitiza mchango kwa wale ambao wamejiunga na umoja huo huku akiwasisitiza ambao hawajajiunga na kikundi kujiunga ili kudumisha umoja baina ya watumishi.
"Sasa katika kikundi hiki tuna miezi Saba mpaka sasa tangu kianzishe sasa kwa watu wanaojiunga kwa sasa tunawakaribisha sana lakini pia kwa wale ambao bado hawajajiunga basi waone umuhimu wa jambo hili na kujiunga " Amesema Lukiza.
Sambamba na ajenda hiyo, kikao hicho kimejadili utekelezaji wa bajeti ambapo katibu wa Afya Ayubu charlse amewataka watumishi wote wa idara ya utawala kuhakikisha wanatekeleza kazi ambazo wameziainisha katika mpango wa bajeti wa mwaka 2025/2026 ili kuhakikisha adhima ya hospitali kupitia idara inatimia.
"Jamani sisi kama wanautawala tunatakiwa kuhakikisha tunatekeleza mipango yote tuliyojiwekea na hili linafanyika kupitia vitengo vyote, hii inamaana kuwa kukamilika kwa shughuli za vitengo kutasaidia kutekeleza mipango ya idara na hospitali kwa ujumla " amesema Ayubu.
Hata hivyo katika kujadili ajenda ya ushirikiano hasa katika suala la kikundi cha M Koba wajumbe mbalimbali wameeleza kulipoke ambapo Bw. Ezekil Togomba kutoka kitengo cha huduma kwa wateja cha Hospitali amesema ni jambo jema kila mtumishi wa idara hiyo hanabudi kulitilia maanani.
‘’Kwanza mimi ni seme tu