TIMU YA KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO YATAKIWA KUENDELEA KUBORESHA HUDUMA.

Posted on: November 13th, 2025

Timu ya kudhibiti na kupambana na magonjwa ya mlipuko Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma imefanya kikao chenye lengo la kujadili mwenendo wa utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa wenye magonjwa ya mlipuko.


Kikao hicho ambacho kimeongozwa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma Dkt. Joseph Nangawe kimejadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoa huduma kuwatayari kuwahudumia wagonjwa hao ambapo Dkt. Nangawe ametoa wito kwa watumishi wote kuhakikisha wanatimiza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi wakiwemo wenye magonjwa ya mlipuko.


“Tumejadili mambo mengi, muhimu ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, kama viongozi hatutarajii kuona au kusikia kwamba kunamgonjwa amekuja Maweni na asipewe huduma kwa sababu ya watumishi kutokuwa tayari kutoa huduma, tukumbuke lengo kubwa la sisi kuwepo hapa nikuwahudumia wanakigoma na watanzania” amesema Dkt. Nangawe.


Hata hivyo Dkt. Boniface Kilangi ambaye pia ni Mratibu wa Huduma za Afya za Hospitali amesema kuwa watoa huduma wote wanao wajibu wakutoa huduma kwa wananchi, ambapo amewataka kuwaona wagonjwa wenye magonjwa ya mlipuko kama wagonjwa wengine ambao wanawahudumia kila siku.


“Tumekua tukitoa huduma bora sana kwa wananchi wanaofika hospitalini kwetu, hivyo hatunabudi kuwahudumia watu wote bila kujali huyu ni mgonjwa wa ugonjwa wa mlipuko kwa  sababu tunatakiwa kuwahudumia kama wagonjwa wengine tunao wahudumia kila siku na hii itasaidia sana kuendelea kuhakikisha tunauishi moto wa hospitali yetu wa huduma bora kipaumbele chetu” amesema Dkt. Kilangi, Mratibu wa Huduma za Afya.


Kwa upande wake Immakulata Malwa kutoka kitengo cha Ubora ambaye pia ni mjumbe wa kikao hicho amewataka watoa huduma kuzingatia kanuni katika maeneo ya kutolea huduma hizo ili kuendele kuweka mazingira rafiki ya kutolea huduma ambapo amesema kuwa jukumu hilo ni lakila mmoja.


“Katika kuhakikisha tunaendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa wenye magonjwa ya mlipuko lazima tuzingatie kanuni za utoaji wa huduma katika maeneo mbalimbali yanayotumika kutolea huduma hizo, hivyo kila mmoja anawajibu wa kulifanya hili ilituweze kufika sehemu ambayo tunahitaji kufika” amesema immakulata.

Pamoja na ajenda mbalimbali kujadiliwa katika kikao hicho, suala la watumishi kuendelea kuhakikisha wanatoa huduma kwa kuzingatia miongozo halijaachwa nyuma ambapo wametakiwa kuhakikisha wanafuata kanuni na miongozo ya utumishi katika maeneo yao ya kutolea huduma.