MGANGA MKUU WA SERIKALI DKT. GRACE MAGEMBE ARIDHISHWA NA UTOAJI WA HUDUMA MAWENI RRH

Posted on: September 16th, 2025



Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe  afanya  ziara mkoani  Kigoma ili kujionea Utayari wa kukabiliana na hatari ya magonjwa ya mlipuko na Utoaji wa Huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mkoa Maweni – Kigoma.


Katika ziara hiyo Dkt. Magembe ametembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma za afya katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma pamoja na maeneo mengine mkoani humo likiwemo eneo la bandari kujionea utayari wa kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na kuwataka viongozi kuendeleza ushirikiano katika udhibiti wa magonjwa hayo.


"Kwa viongozi. akiwemo Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Damas Kayera ,Mganga Mfawidhi  wa Hospitali  Dkt. Joseph Nangawe naomba mchukue hatua za makusudi katika kushirikiana ili  kuendelea kuboresha huduma na kutoa huduma bora kwa wananchi wa Kigoma, eneo hili limepakana na nchi jirani hivyo tunahitaji udhibiti wa magonjwa kwa sababu mwingiliano nimkubwa sana."amesema Dkt. Magembe Mganga Mkuu wa Serikali.


Katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni - Kigoma Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt.Damas Kayera amesema Mkoa kupitia ofisi yake imejipanga kuhakikisha huduma za Afya katika Mkoa hasa Hospitali ya Mkoa na vituo mbalimbali vilivyoko ndani ya Mkoa zinaendelea kuboreshwa zaidi ili kuweza kuwanufaisha wananchi wa Kigoma na kueleza jitihada zinazofanywa na mkoa katika kudhibiti magonjwa ya mlipuko.

 

"Mkoa tumejipanga kuhakikisha huduma bora zinaendelea kutolewa, katika hositali ya Mkoa yamefanyika mapinduzi makubwa upande wa vifaa tiba na watumishi, hivyo tutaendelea kuboresha,  lakini upande wa vituo vya afya pia huduma zimeboreka sana, kama mkoa tayari tumechukua hatua katika maeneo ya bandari uwanja wa ndege,kituo cha mabasi  pamoja na maeneo ya mipaka kwa kuweka vituo vya huduma ili kudhibiti magonjwa hayo ya mlipuko. Amesema Dkt. Damas.


Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni _ Kigoma Dkt.Joseph Nangawe ameeleza kuwa Hospitali ina mipango ya kuendelea kuboresha huduma, kama ujenzi wa wodi ya wazazi (Martenity Complex) na kuongeza kuwa ipo miradi ambayo imekamilika kwa sasa imekua msaada mkubwa katika utoaji wa hudma kama uzalishaji wa hewa tiba na kuiomba wizara kuendelea kusimamia maboresho ya miundombinu katika hospitali hiyo.


“Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe sisi kama hospitali tunajivunia sana maendeleo ya huduma katika hospitali yetu, tulikua tunasumbuliwa sana na upatikanaji wa hewa tiba ambayo tulikua tukifuata Mwanza lakini kwa sasa tunazalisha hapa lakini pia miradi kama ujenzi wa jengo la wagonjwa  nje (OPD) ambalo kwa sasa tunalitumia na kutusaidia sana, hivyo tunaamini wizara inaenda kumalizia ujenzi wa jengo hilo.  Amesema Dkt.Nangawe.