MAWENI RRH YAJIPANGA KUIMALISHA USAFI KATIKA MAENEO YOTE

Posted on: September 12th, 2025
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni – Kigoma imefungua ukura mpya wa uimarishaji wa mazingira kwa kuingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya usafi ya Jodata ambayo itashughulikia masuala yote ya usafi ndani ya Hospitali chini ya usimamizi wa kitengo cha Afya mazingira cha hospitali.
Mktaba huo wenye lengo la kuimalisha hali ya usafi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni –Kigoma umefanyika kufuatia tamati ya makata wa kampuni ya awali iyokuwa ikisimamia usafi ndani ya hospitali na kuifanya hospitali kuchukua jukumu la usimamizi kwa kuajili watumishi wa usafi. 



Hata hivyo ujio wa kampuni ya Jodata umewafanya Wafanyakazi wa usafi wa hospitali ya rufaa mkoani kigoma-Maweni kufurahi baada ya kupokea vifaa vya usafi kutoka kwa kampuni hiyo mpya lengo likiwa ni kupunguza magonjwa ya kuambukiza na kudumisha usafi wa hospitali na kuweka mazingira rafiki wa wagonjwa . 


“Tunaiomba kampuni yetu iwe inatoa vifaa kwa wakati ili kutoka chini kwenda juu, sisi ni wapambanaji tunaamini kupitia kampunii hii tutafanya zaidi tutatoka sehemu ya tatu hadi ya kwanza” amesema Elizabeth Vicent ambae ni mmoja wa wafanyakazi pia kiongozi katika kampuni hiyo ya usafi.


Pia baadhi ya watumishi wapya wameeleza matumaini yao huku wakiahidi kuhakikisha Maweni inaendelea kuwa safi pia wameuomba uongozi wa hospitali kuendele kutoa ushirikiano ili kuweka mazingira rafiki ya kazi ili kufikia malengo yaliyo wekwa na kampuni pamoja na hospitali katika suala la usafi.


“Mimi nimejiunga huu ni mwezi wangu wa kwanza hapa lakini kazi ni nzuri nafurahia kwanza kabisa imeinua kipata changu naamini ntatoka sehemu moja kwenda nyingine, lakini naiomba kampuni ihakikishe inatuwekea mazingira rafiki ili tuweze kufanya vile ambavyo inatakiwa kama ambavyo wamefanya katika mwezi huu wa kwanza kwakweli wanajitahidi na mimi ntapambana”amesema Philipo. 


Aidha, Afisa mazingira waHhospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Simon Willison amesema watahakikisha kila mfanyakazi anakuwa na vifaa vyote vya kazi kama buti na maski na kutatua changamoto za wafanyakazi kwa wakati huku akiweka bayana kuwa lengo la hospitali ni kuhakikisha mazingira yote yanakua safi na kupanda kutoka nafasi ya tatu kitaifa kati ya hospitali 28 .