MAWENI RRH YAENDESHA MAFUNZO YA AFYA YA AKILI KWA WATUMISHI
Posted on: September 12th, 2025
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma kupitia kitengo cha Afya ya akili imeendesha mafunzo ya Afya ya alkali na msaada wa kisaikolojia mahala pakazi kwa siku tano kwa watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni- Kigoma.
Mafunzo hayo ambayo yameanza kufanyika tarehe 8/09/2025 na kutarajiwa kumaliza siku ya ijumaa ya tarehe 12/08/2025 katika ukumbi wa mikutano wa Maweni (Binagi Hall) yanatarajia kuwanufaisha watumishi zaidi ya 365 ndani ya siku zote tano.
Pia Hellen F. Mrema Msaikolojia tiba (clinical psychologist) ambaye ni mkufunzi wa mafunzo hayo ameeleza vitu mbalimbali vikiwemo msongo wa mawazo ambapo amesema watu wengi wanchanganya msongo wa mawazo (stress) na vitu vingine, ambapo amesema kuna hatua zake ambazo ni msongo wa mawazo ya kawaida, msongo wa mawazo ya kiwango cha kati pamoja na msongo wa mawazo uliyo pitiliza na kusema kuwa msongo wa mawazo ni jambo ambalo kila mtu anayo lakini yakizidi ndiyo huleta shida.
“Watu wanachanganya sana ila ukweli ni kwamba kila mtu ana msongo wa mawazo hivyo si kila msongo wa mawazo ni tatizo bali msongo wa mawazo uliozidi huwa ndiyo tatizo na hapo ndipo tunasema mtu huyu anahitaji mtaalamu” amesema Hellen Msaikolojia tiba.
Katika mafunzo hayo Hellen F.Mrema amesema msongo wa mawazo hupelekea vitu vingi ikiwemo watu kuchukua maamuzi yasiyofaa kama kujiua au kujidhuru wenyewe na katika kuthibitisha hilo ameeleza kuwa, kutokana Na magonjwa ya afya ya akili Zaidi ya watu laki 7 duniani wanakufa kutokana na kujiondoa uhai ambapo miongoni mwao asilimia (20%) ya watu hutumia Sumu Kama njia kuu katika kujiondoa uhai, (kutokana na tafiti za shirika la afya duniani).
“Ukweli wanaume wengi wanafanya tendo hilo la kujitoa uhai na huku asilimia chache ya wanawake wanajaribu kujiondoa uhai katika maeneo ya vijijini kutokana na kukosa baadhi ya mahitaji kama vile; chakula, malazi na mavazi na huduma nyingine watoto yatima na watoto wa waishio katika mazingira magumu na kupotea”amesema Hellen.
Mwisho ametoa ushauri kwa wafanyakazi wote na kuwahimiza kuwasaidia wagonjwa ambao tayari wamefikia hatua hiyo na ameendelea kuzungumza njia muhimu za kuwasaidia kutokana na mambo mbalimbali ikiwemo Mawazo kwa kuwapatia ushauri nasaha ,kupata muda mwingi wa kupumzika na kupenda kutembelea sehemu mbambali kwani husaidia kuondoa mawazo mabaya, “Watu wengi wako bize sana hawana muda wa mapumziko jambo ambalo ni baya watu hawatembei kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, lakini pia kula vizuri na mambo mengine mengi hivyo tufanye hivyo ili kulinda afya zetu za akali”amesema Hellen.