BODI YA USHAURI YA HOSPITALI YAKAA KUJADILI UTEKELEZAJI WA SHUGHULI KATIKA ROBO YA TATU, 2025/2026

Posted on: April 24th, 2026

Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni - Kigoma imefanya kikao chake cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha, 2025/2026 lengo likiwa ni kujadili utekelezaji wa shughuli mbalimbali zililizopangwa kufanyika katika kipindi hicho.

Katika kikao hicho taarifa mbalimbali ikiwemo taarifa ya utekelezaji wa kitengo cha uhasibu na fedha imewasilishwa, huku ikionyesha kuwa makusanyo ya Hospitali hiyo yameongezeka kwa 12% ikilinganishwa na robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026.

Akiwasilisha taarifa hiyo Kaimu mkuu wa kitengo cha uhasibu na fedha Cpa(t) Reginald Hhayuma amesema ungezeko la mapato hayo limetokana na sababu mbalimbali ikiwemo ujio wa wataalamu ( mabingwa ) kutoka nje ya hospitali hiyo pamoja na uboreshwaji wa huduma katika vitengo mbalimbali hospitalini.

"Mhe. Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya Hospitali pamoja na wajumbe, kwa robo ya tatu makusanyo ya hospitali yameongezeka kwa asilimia 12 ikilinganishwa na robo ya pili sababu kubwa ikiwa ni ufuatiliaji wa makusanyo ya bima pamoja na kuazima madakatri bingwa kutoka nje ya hospitali kwenye baadhi ya maeneo" amsema Cpa(t) Reginald Hhayuma.